1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wanafunzi 280 watekwa nyara Nigeria

8 Machi 2024

Watu waliojihami kwa bunduki wamewateka nyara zaidi ya wanafunzi 280 baada ya kuivamia shule kaskazini magharibi mwa Nigeria katika mojawapo ya visa vikubwa zaidi vya utekaji nyara kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4dIhm
Nigeria | Utekaji nyara wa Shuleni 300  huko
Watu hukusanyika kwenye eneo ambalo watu wenye silaha wamewateka nyara mamia ya watoto wa shule, Picha: AP/dpa/picture alliance

Maafisa wa serikali katika jimbo la Kaduna wamethibitisha utekaji nyara huo katika shule ya Kuriga hapo jana, ila hawakutoa idadi kamili. Mmoja wa walimu katika shule hiyo iliyoko mkoa wa Chikun Sani Abdullahi, amesema walimu walifanikiwa kutoroka na wanafunzi wengi wakati wavamizi hao walipokuwa wakifyatua risasi hewani. Mkaazi wa eneo hilo Mohammad Adam ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba, zaidi ya watoto 280 ndio waliotekwa nyara baada ya kufanya hesabu kwa umakini zaidi. Kwa kawaida idadi ya waliotekwa nyara Nigeria hurudi chini baada ya waliokimbia uvamizi kurudi makwao.