1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika wampongeza Diamaye Faye kwa ushindi Senegal

Amina Mjahid
29 Machi 2024

Umoja wa Afrika umempongeza mgombea wa urais wa upinzani nchini Senegal Bassirou Diomaye Faye, kwa ushindi katika uchaguzi wa urais uliomalizika nchini humo na kuyakubali matokeo ya uchaguzi huo.

https://p.dw.com/p/4eFYc
Bassirou Diomaye Faye
Mgombea wa urais wa upinzani nchini Senegal Bassirou Diomaye FayePicha: Luc Gnago/REUTERS

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo Moussa Faki Mahamat amempongeza Faye kwa ushindi na kumtakia mafanikio.

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi yanampa Faye ushindi wa asilimia 54.3 ya kura akimpiku mgombea wa chama tawala, aliyewahi kuwa waziri mkuu Amadou Ba, aliyeungwa mkono na rais anayeondoka Macky Sall. 

Rais Macky Sall akutana na rais mteule Diomaye Faye

Mahakama ya katiba ya Senegal inaweza kumtangaza Faye aliye na miaka 44 kuwa mshindi wa uchaguzi kabla juma hili kukamilika na hatua ya kukabidhi madaraka itafanyika kabla ya Aprili 2, ambayo ni tarehe rasmi ya kumalizika kwa muhula wa Macky Sall madarakani.