1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Japan kuanza tena kulifadhili shirika la UNRWA

Amina Mjahid
29 Machi 2024

Serikali ya Japan imesema inajitayarisha kuanza tena kulifadhili shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA linaloratibu misaada yote inayoingia Gaza.

https://p.dw.com/p/4eFai
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA
Japan kuanza tena kuifadhili UNRWA baada ya kukutana na mkuu wa shirika hlo mjini TokyoPicha: Mahmoud Issa/ZUMAPRESS/picture alliance

Japan ambayo ni mfadhili mkubwa wa sita kwa shirika hilo, iliungana na mataifa mengine kusimamisha kwa muda msaada wake kwa UNRWA, baada ya Israel kudai kuwa wafanyakazi 12 kati ya 13,000 wa shirika hilo, walihusika katika shambulizi la Oktoba 7 kusini mwa Israel lililofanywa na wanamgambo wa Hamas. 

UN: Nusu ya wakaazi wa Gaza wanakabiliwa na baa la njaa

Awali waziri wa mambo ya nchi za nje wa Japan Yoko Kamikawa alikutana na mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini mjini Tokyo kujadili hatua zilizochukuliwa na shirika hilo kuimarisha utawala bora na uwazi. 

Japan imesema ufadhili huo uliosimamishwa mwezi Januari utaanzishwa tena mwezi Aprili. Australia, Canada, na Sweden pia zilitangaza mwezi huu kuanza tena kulifadhili shirika la UNRWA.