| 30.07.2010 | 10:00 UTC
Idadi ya wasio na kazi yapanda
Wakati huo huo , idadi ya watu ambao hawana ajira imepanda kwa kiasi cha watu 39,000 katika mwezi wa Julai ikilinganishwa na mwezi uliopita. Lakini idara ya kazi nchini Ujerumani imesema kuwa uchumi unarejea katika hali nzuri, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita, hivi sasa kuna watu wachache zaidi ambao hawana ajira. Kiwango cha watu wasio na ajira kinafikia asilimia 7.6, ambapo watu milioni 3.2 wamejiandikisha kuwa hawana ajira. Wiki iliyopita , kiashirio cha hali ya biashara kinachofuatiliwa sana cha IFO, kilipanda kwa kiwango cha juu katika muda wa miaka mitatu na kuashiria kuwa makampuni ya Ujerumani yanamatumaini makubwa ya hali ya baadaye.






